ZANZIBAR INAFURSA KUBWA YA KIBIASHARA KARIBUNI WAFANYABIASHARA.
- January 8, 2026
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, leo amekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (ZITF) yaliyofanyika katika viwanja vya maonesho, yakihudhuriwa na viongozi wa serikali, wafanyabiashara, wawekezaji pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya biashara.
Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amewahimiza wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza na kufanya biashara Zanzibar, akibainisha kuwa Zanzibar ina mazingira rafiki ya uwekezaji, fursa nyingi za kiuchumi pamoja na sera zinazounga mkono maendeleo ya sekta binafsi. Aidha, amesisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia katika biashara ili kuongeza ufanisi, kupanua masoko na kukuza ushindani wa bidhaa na huduma, akieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa matumizi ya teknolojia katika kukuza uchumi.
Sanjari na hayo Mhe. Mgeni rasmi amewapongeza waandaaji wa Maonesho hayo TanTrade kwa kushirikiana na Unique Touch na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Biashara Zanzibar.