KAMISHNA WA POLISI ZANZABAR ATEMBELEA SABASABA 2025.
- July 5, 2025

5 JULAI, 2025.
Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Kombo KH. Kombo amefika leo kwenye kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere (Sabasaba Grounds) kwa lengo la kutembelea Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayotoa fursa ya kuona, kujifunza na kununua bidhaa na huduma mbalimbali, za wafanyabiashara, wajasiriamali na wawekezaji wa ndani na nje wanaoshiriki Maonesho haya katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.