Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

Maonyesho ya Bidhaa za Kuagiza ya Yiwu 2023 yanaendelea kwa siku ya pili ambapo watembeleaji na wawekezaji walivutiwa na bidhaa na huduma mbalimbali za Tanzania

  • November 14, 2023

Novemba 14, 2023
 
Yiwu, Zhejiang-
 China .
 
Maonyesho ya Bidhaa za Kuagiza ya Yiwu 2023
 yanaendelea kwa siku ya pili ambapo watembeleaji na wawekezaji walivutiwa na bidhaa na huduma mbalimbali za Tanzania.

Kwa upande wa Sekta ya Utalii Bw. Charles Bekoni ambaye ni Muanzilishi na Mmiliki wa Masailand Arusha alitoa maelezo mengi ya kina kuhakikisha wachina wengi wanaongeza idadi ya kutembelea vivutio mbalimbali ikiwamo kuona mbuga za Serengeti, Ngorongoro na kuona vivutio vilivyopp Zanzibar.

Bw. Bekoni ameweza kupata ahadi za watalii tofauti kuonyesha nia ya kutaka kuja kutembelea Tanzania na kuona vivutio vilivyomo nchini.

Aidha, Bi. Samira Mohamed, Afisa Biashara kutoka TanTrade alipata nafasi ya kuzungumza na mmoja ya mtembeleaji katika Banda Bw. Shareef, Meneja ABC Factory China ambaye ameonesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania.

Vilevile Bi. Jenipha Japhet Lulabohotse, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Rhinoceros alipata nafasi kuzungumza na vijana wa kitanzania waishio China waliotembelea Banda la Tanzania leo na kuwashauri kuwekeza TANZANIA 🇹🇿