Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

WAZIRI JAFO AELEZEA MAFANIKIO MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA

  • May 15, 2025

15 Mei, 2025
Dodoma


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb) amebainisha mafanikio mbalimbali iliyopata wizara kwa  kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya Sita ikiwemo kuongezeka kwa Viwanda ambavyo vimeongeza ajira kwa watanzania. Pia amesema kuwa Wizara imeweza kuwezesha wafanyabiashara wa kitanzania kupeleka bidhaa zao katika maonesho mbalimbali ya kimataifa kama vile maonesho ya mboga mboga , Maonesho ya AFTA na hata Maonesho ya ndani ya nchi ambayo yanajulikana kama Sabasaba ambayo yanafanyika kila mwaka ambayo yamekuwa mchango mkubwa sana kwa wafanyabiashara.