Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

WATUMISHI WA TANTRADE WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

  • March 10, 2025

Watumishi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) leo tarehe 8 Machi, 2025 wameungana kwa pamoja katika viwanja vya Leaders Club, Jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha na kusheherekea Siku ya Wanawake duniani.

Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu inayosema "Wanawake, Wasichana 2025 tuimarishe Haki Usawa na Uwezeshaji". Kauli mbiu hii imelenga kuhamasisha maswala ya haki, usawa na uwezeshaji katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na kijamii.