Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

Mamalaka ya Maendeleo ya Bishara Tanzania (TanTrade) yaendelea kuitangazaTanzania katika Maonesho ya Dunia ya Mbogamboga na Matunda

  • November 10, 2023

Doha, Qatar

Mamalaka ya Maendeleo ya Bishara Tanzania (TanTrade) yaendelea kuitangazaTanzania katika Maonesho ya Dunia ya Mbogamboga na Matunda #expo2023doha.

Watembeleaji kutoka mataifa mbalimbali likiwemo Ujerumani wametembelea Banda la Tanzania na kuipongeza Tanzania kuwa moja ya sehemu bora ya Utalii Duniani. Watembeleaji hao wamepanga kutembelea Tanzania kati ya mwezi Januari na Februari, 2024 ambapo wataweza kutembelea Zanzibar na Mbuga ya wanyama ya Mikimu na kuomba kuunganishwa na kampuni sahihi za utalii ili kuwezesha ziara hiyo.

Kwa upande wa Maafisa kutoka TanTrade, wamewapongeza na kuwakaribisha watu hao kutembelea Tanzania na kuwaahidi kuwa TanTrade itawaunganisha na kampuni sahihi za utalii ili kuhakikisha malengo ya safari yao yanafikiwa. Sekta zingine zinazotangazwa katika Maonesho hayo ni kilimo, madini, na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini.

#tukutaneexpo2023doha
#expo2023doha