TanTrade na ZIPA Kushirikiana Kutangaza Uwekezaji na Biashara Zanzibar
- November 14, 2024
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na Mamlaka ya Uwekezaji ya ZIPA wameanzisha mkakati wa pamoja wa kutangaza vivutio vya uwekezaji na fursa za biashara Zanzibar. Katika kikao tarehe 12 Novemba 2024 kwenye ofisi za ZIPA, Msimamizi Mkuu wa Ofisi ya TanTrade Zanzibar, Bw. Tahir Mussa Ahmed, alieleza kuwa watafanya kazi na ZIPA kuhakikisha fursa hizo zinajulikana ndani na nje ya nchi na kuzitafutia masoko bidhaa na huduma za Wawekezaji wa Zanzibar nje ya Nchi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa ZIPA, Nd. Saleh Saad Mohamed, alibainisha kuwa ZIPA inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji, jambo linalovutia wawekezaji wa ndani na nje katika sekta mbalimbali. Alisisitiza umuhimu wa kuongeza nguvu na kushirikiana katika kuitangaza Zanzibar ili kuhakikisha fursa za kimkakati zinajulikana kwa watu wengi zaidi kupitia njia mbalimbali za matangazo.