Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

Uchaguzi tarehe 29 Oktoba, 2025

Kura yako haki yako, jitokeze kupiga kura

Uchaguzi 2025

SANAA YA TINGATINGA RASMI KUTUMIA NEMBO YA MADE IN TANZANIA.

  • October 13, 2025

Mchoraji wa Kimataifa wa Sanaa ya Tingatinga Bw. Michael Yusuph Lehemu amekabidhiwa cheti cha kutumia Nembo ya Made in Tanzania ili kutambulisha Sanaa ya Tingatinga katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Wakati akikabidhi cheti hicho Bw. Baltazari Joseph, Afisa Mwandamizi kutoka TanTrade alieleza kuwa Michoro ya Tingatinga ni Sanaa pekee duniani inayopatikana Tanzania, hivyo ni muhimu kulinda kazi hizi za Sanaa kwa kuiwekea utambulisho wa nembo ya Taifa ya Made in Tanzania ili kutambulika kimataifa na kulinda ubunifu wa Wasanii wa Tanzania.

Kwa upande wake, Bw. Lehemu ameishukuru TanTrade kwa kumpatia elimu ya matumizi ya Nembo ya Taifa na kuahidi kutumia nembo hiyo katika kazi zake za Sanaa. Vilevile ameishukuru TanTrade kwa kumwezesha kushiriki katika Maonesho mbalimbali ya Kimataifa kutangaza kazi zake za Sanaa ikiwemo Maonesho ya Aichi Expo 2005, Shanghai Expo 2010, Yeosu Expo 2012, Milan Expo 2015 na sasa Expo 2025 Osaka,