SIKU YA TATU YA MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA SABASABA 2025.
- July 1, 2025

1 JULAI, 2025.
Watanzania na wageni mbalimbali wanaendelea kujitokeza ilikujionea makubwa waliyoandaliwa na wafananya biashara wa Kitanzania pamoja na wakigeni kwenye maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2025). Maonesho haya ya Kimataifa yamelenga kuwainua wafanyabiashara wa Kitanzania kwa lengo la kuwafungulia milango ya biashara, kubadilishana uzoefu, kuwakutanisha na wadau wa mabenki, kuwakutanisha wateja wapya sambamba na kujifunza mbinu mbalimbali za masoko, Maonesho ya Sabasaba yanafanyika katika kiwanja cha Mwl. J. K. Nyerere (Sabasaba Grounds) barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.