Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

KONGAMANO LA TATU LA WAKUU WA TAASISI LAFUNGULIWA RASMI ZANZIBAR

  • January 7, 2025

06 Januari 2025.

Zanzibar

Makamu wa pili wa Rais wa Serikari ya Mapindunzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amefungua rasmi kongamano la Tatu  la Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Serikari ya Jamuruhuri ya Muungano wa Tanzania na Taasisi za Serikari ya Mapindunzi ya Zanzibar huku akihamasisha ushirikiano wa taasisi za umma katika kongmano lililofanyika leo katika ukumbi wa Golden Tulip, Zanzibar.

Aidha Makamu wa pili wa Rais wa Serikari ya Mapindunzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa rai kwa Taasisi toka pande zote mbili kutumia jukwaa hilo kufanikisha ufanisi katika utendaji na kutumia Jukwaa hilo kutatua kero za kimuungano kwa manufaa na maendeleo ya kiuchumi kwa watanzania huku aikitaka serikali ya  Mapinduzi ya Zanzibar kuandaa jukwaa la namna hii.