Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

KAMATI YA WAZIRI MKUU IMEKUTANA NA TAASISI ZA KIKODI NA UDHIBITI NCHINI.

  • July 21, 2023



..............................
Na. Norah Thomas-Dar es salaam.
23 Mai, 2023.

Kamati maalum ya kupitia changamoto za kibiashara nchini iliyoundwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa imeendelea kukutana na Mamlaka zinazohusika Kodi na udhibiti nchini.

Kwa siku mbili za tarehe 23 na 25 Mei, 2023 kamati imekutana na Mamlaka ya Mapato (TRA) ,Mamlaka ya Bandari (TPA), Shirika la Viwango nchini (TBS) Pamoja na Tume ya Ushindani nchini (FCC).

Pamoja na mambo mengine tume ilitaka kupata kiini cha changamoto za kibiashara chini kama iilvyoibuliwa na wafanyabishara katika kikao chao na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt.John Jingu amesema Kamati imeendelea na utekelezaji wa majukumu yake ambapo siku ya tarehe 23 kamati ilifika Bandarini eneo ambalo mizigo inapakuliwa na kuhifadhiwa na baadae Kamati imetembelea Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kukutana na Wadau mbalimbali wanaohusika na forodha.
Dkt. Jingu amesema Kamati imefanikiwa kuendela kukusanya maoni na kufanya mahojiano na Wataalam hao ambapo wametoa maoni mazuri yatakayosaidia kutatua changamoto zilizopelekea kuleta mgogoro na Wafanyabiashara.

Kamati pia imefanya mahojiano na wawakilishi wa makundi ya Wafanyabiashara na Wadau mbalimbali ambao hawakuweza kupata nafasi ya kutoa maoni kwenye mkutano wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasimu Majaliwa na Wafanyabiashara uliofanyika tarehe17 Mei , 2023 Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Jumuhia ya Wafanyabiashara nchini Bw,Hamis Livembe aliwataka taasisi na Mamlaka zinazofika mbele ya kamati kujikita katika kutafuta ufumbuzi zaidi badala ya kujitetea kwa kusimamia sheria za Mamlka husika.
‘’Ndugu zangu ,sisi siyo mahakama, nawaomba sote kwa Pamoja tujikite kwenye kutafuta suluhu ya changamoto zilizopo badala ya kila anayeitwa mbele ya kamati ama kujitetea au kutaja sheria za mamlaka au taasisi yake’’ alisisitiza Bw.Livembe.