Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA KUPITIA TANTRADE NA BODI YA UDHIBITI NA USIMAMIZI WA MFUMO WA STAKABADH ZA GHALA (WRRB) WATOA WITO KWA WAKULIMA KUTUMIA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA ILI KUPANUA MASOKO

  • August 7, 2023

......................................
Na. Norah Thomas- Manyara.
5 Agusti,2023.


Hayo yamesemwa tarehe 5 Agusti, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga alipokuwa kwenye kikao cha uzinduzi wa  Matumizi ya mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwenye zao la Mbaazi na Vitunguu Swaumu kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Kikao hicho kina lengo la kupitia kwa pamoja mwongozo wa uuzaji wa mazao jamii ya Kunde kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala,  pia kilihusisha wadau mbalimbali wakiwemo , Wakuu wa wilaya , wakulima na waendesha Maghala Pamoja na Taasisi za Serikali na Binafsi, 
Aidha Mhe. Sendiga  aliwaasa wakulima kutumia mfumo huo ili kuongeza ubora wa mazao na hivyo kupelekea kuongezeka kwa bei sokoni na kuongeza faida kwa Mkulima na wadau wengine. Pia alisisitiza wadau wote katika mfumo huo kutimiza wajibu wao ili kuepusha changamoto zozote zinazoweza kujitokeza. Pia alizindua rasmi matumizi ya mfumo wa stakabadhi za ghala katika mazao ya Mbaazi na Vitunguu Saumu katika msimu wa 2023, hata hivyo alieleza kuwa maandalizi yanaendelea kwa ajili ya kutumia mfumo huo katika zao la Dengu na wadau watatangaziwa pindi maandalizi yakikamilika.



Nae  Afisa Biashara kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)  Bi. Grace Simbakavu kwa niaba ya Mkurugenzi  Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Khamis,  alisema kuwa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala una faida kubwa na manufaa kwa Mkulima kwani husaidia  katika kuboresha uchumi binafsi na Taifa kwa ujumla. Pia   alisisitiza, TanTrade  ipo tayari kuhamasisha  Wakulima watumie mfumo huo  kwani ni njia salama na unasaidia kuleta kipato cha uhakika kwa Mkulima, na alisistiza kuwa kwa kutumia mfumo huu utamsaidia mkulima kutoangaika kutafuta masoko ya bidhaa zake anazozalisha kwani Serikali kupitia TanTrade itawajibika katika kupata masoko ya bidhaa zao.

Pia alisistiza kuwa, TanTrade itatoa  usaidizi wakati wowote kwa ajili ya kufanikisha matumizi ya mfumo huo, na kutoa wito kwa Wadau wote wa Kilimo kwa  pamoja kuridhia matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala katika Mikoa  yao.

‘’Mhe. Rais Dkt. Samiah Suluh Hassan,  ameweka umakini mkubwa kwa sekta ya Kilimo kwani sekta hii ndio mkombozi wa Watanzania, hivyo Natoa wito kwa Wadau wote wa Kilimo kuunga mkono jitihada zinazowekwa na Serikali  ambapo ni Pamoja na  mifumo mbalimbali inayozinduliwa ili kuinua uchumi  na kuendelea  kukuza sekta ya kilimo, kwani matumizi ya mifumo rasmi  katika mauzo ya bidhaa mbalimbali ni nyenzo muhimu ya upatikanaji wa masoko ya uhakika na kupata bei halisi ya soko kwa bidhaa husika wakatu huo’’. Alisema.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw. Asangye Bangu alisema kuwa Bodi iko tayari kutoa usaidizi wakati wowote kwa ajili ya kufanikisha matumizi ya mfumo huo, pia aliongeza kuwa Wadau wote kwa pamoja wameridhia matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala katika Mkoa wa Manyara.