Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AFUNGA RASMI MAONESHO YA WIKI YA VIWANDA NA BIASHARA

  • May 22, 2024

22 Mei 2024
Dodoma.

Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji leo amefunga rasmi maonesho ya Viwanda na Biashara yaliyokuwa yakifanyika katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Katika hotuba yake ya kufunga rasmi Maonesho hayo Mhe. Waziri amesema Uchumi wa taifa unabebwa na viwanda na biashara huku akisisitiza kuwa idadi kubwa ya walioajiriwa katika Sekta  viwanda na biashara ni vijana.

Mhe. Waziri aliongezea kuwa Wizara inaandaa Mkakati wa Biashara kidijitali ambao unalenga katika kuhakikisha wafanyabiashara wanatumia teknolojia katika kufanya biashara na kuwataka wafanyabiashara wawe waaminifu kwa wateja wanapofanya biashara mtandaoni.

Kwa upande mwingine Naibu waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amesema ubunifu huu wa kufanya maonesho ya Viwanda na Biashara uendelee kwasababu Waheshimiwa wabunge wamepata fursa ya kufahamu mambo mbalimbali yanayohusu Wizara, taasisi zake na kampuni mbalimbali zinazozalisha na kufanya biashara nchini.