Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MISRI WATEMBELEA BANDA LA TANZANIA-MAONESHO TATU YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA AFRIKA(3rd IATF)

  • November 12, 2023

Leo tarehe 12 Novemba, 2023 Maofisa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Misri walitembelea banda la Tanzania kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Afrika (IATF) ambapo walijadili kwa pamoja na maafisa waandamizi wa Taasisi mbalimbali za Serikali ya Tanzania juu ya Utekelezaji wa fursa mbalimbali za masoko yaliyopatikana ya bidhaa zinazozalishwa nchini Tanzania na Wawekezaji walionesha nia ya kuwekeza nchini Tanzania.
Katika Maonesho haya ya 3 ya IATF, ushiriki wa Tanzania unaratibiwa na TANTRADE ambapo taasisi mbalimbali na Sekta Binafsi zinashiriki.