WATANZANIA WAALIKWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATIKA JIMBO LA HARYANA NCHINI INDIA
- July 25, 2023

………………….
Na. Norah Thomas-TanTrade Dar es salaam.
Dar es salaam
10 Julai, 2023.
Hayo yameyasemwa leo tarehe 10 Julai, 2023 na Katibu Mkuu wa Serikali katika jimbo la Haryana Dkt. Raja Sekhar Vundru Katika Uzinduzi wa siku Maalumu ya Haryana katika Maonesho ya sabasaba, inayofanyika katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl. JK Nyerere barabara ya Kilwa Dar es salaam yenye lengo la kuonyesha fursa za Biashara na Uwekezaji zinazopatikana nchini India katika Jimbo la Haryana pamoja na fursa zinazopatikana nchini Tanzania.
Akizungumza katika Maazimisho ya siku hiyo Dkt. Raja amesema, Jimbo la Haryana limejipanga kufanya Biashara na kuwekeza nchini Tanzania hususani katika sekta ya elimu, Mashine, kilimo, Afya pamoja na Sekta ya Matunda, Pia wanataka kutangaza huduma za TEHAMA, madini na kilimo katika nchi za Afrika, ameongeza kuwa Matunda aina ya Parachichi kutoka Tanzania yana soko sana nchini India, hivyo amewaasa Watanzania kuchangamkia fursa hiyo.
‘’Natoa rai kwa Watanzania kutumia fursa zinazopatikana nchini India katika jimbo la Haryana hususani katika biashara ya Parachichi na matunda mengine kwani Parachichi kutoka Tanzania huwa hazitozwi kodi hivyo tutumie fursa hiyo ili kuzisogeza nchi zetu mbele’’ alisema.
Pia aliongeza kuwa Serikali ya India inatoa Mualiko kwa Wafanyabiashara wa Tanzania kwenda kufanya Biashara na kujionea fursa nyingi zinazopatiana katika jimbo la Haryana, kwani kuna fursa nyingi za biashara na wametengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya biashara na uwekezaji pia wanajenga madaraja ya mahusinao kati ya jimbo la haryana na nchi nyingine ili kusaidia nchi za nje kutumia fursa kujenga mahusiano yatakayokuwa endelevu.
Aidha Mwenyekiti wa Bodi ya Tantrade Profesa Ulingeta O. Mbamba aliongeza kuwa katika kuadhimisha siku ya India katika Maonesho 47 ya DITF, tumetambua na kuona umuhimu wa nchi hii kwani India ni nchi ya tatu (3) kwa kufanya biashara na Tanzania, na thamani ya biashara kati ya Tanzania na India imefikia kiwango cha dola bilioni 4.58 katika kipindi cha mwaka 2021 mpaka 2022.
‘’ Pamoja na kuwa India ni miongoni mwa nchi tunayofanya nayo biashara kwa miaka mingi, pia India ndio nchi yenye jamii kubwa ya Wageni wanaoishi nchini hivyo Serikali ya Tanzania kupitia TanTrade itahakikisha inadumisha Mahusiano mazuri ya kibiashara yaliyopo baina ya Tanzania na India, pia TanTrade itasimamia kwa vitendo Mikataba ya biashara na India.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Bi. Latifa Khamis amesema anaishukuru sana Serikali ya India kwa kudumisha Mahusiano mazuri na Tanzania, na kwa kupitia Mahusiano hayo yamesaidia kuwepo Makampuni zaidi ya 50 kutoka jimbo la Haryna ili kuonesha fursa zilizopo katika jimbo la hilo ambalo linaongoza katika uchumi wa India.
‘’ Msafara huu umekuja na Makampuni zaidi ya hamsini (50) na viongozi kutoka katika Serikali ya India jimbo la Haryana waliohudhulia katika Maonesho haya ya 47 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam (DITF 2023), kuleta bidhaa zao mbalimbali kwa ajili ya kuonesha na kupata wadau wa kufanya nao Biashara, pia kupitia Maonesho haya tumepata mafanikio ya kutia saini Mikataba mikubwa baina ya Serikali zote mbili hivyo natoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kuja kujifunza Teknolojia mpya ya uzalishaji wa bidhaa kutoka kwa wageni wetu mbalimbali’’ alisema.