Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

WATANZANIA WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI ZILIZOPO NCHINI IRANI

  • July 25, 2023

............................

Na. Norah Thomas-TanTrade Dar es salaam.
1 JULAI,2023.

Hayo yamesemwa leo  1 Julai, 2023 na  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania (TanTrade)  bi.Latifa M. Khamis katika hafla ya Maazimisho ya siku ya Iran iliyofanyika katika Uwanja wa Maonesho  wa Mwl. J.K Nyerere katika  kipindi  cha  Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (almaarufu kama SabaSaba) yaliyoanza  tarehe 28 Juni - 13 Julai, 2023. Maazimisho hayo yana lengo la kutangaza fursa za biashara na Uwekezaji  zilizopo nchini Iran na Tanzania ambazo zipo katika sekta  ya Utalii, elimu, Viwanda pamoja na sekta ya Afya.

Bi. Latifa  ameendelea kusema kuwa  Tanzania imekuwa na Mahusiano ya kidipromasia na Utamaduni na nchi ya Iran kwa  Zaidi ya miaka arobaini (40) hivyo TanTrade inahamasisha Watanzania  kutumia fursa za biashara na Uwekezaji  zilizopo nchini  Iran ambazo zinapatikana  katika sekta ya Afya, Viwanda na Kilimo pia wana huduma za wateja nzuri pamoja na uwezeshaji wa biashara na  unafuu  wa  ghalama za  kuendesha biashara.

‘’ TanTrade inaendelea kudumisha Mahusiano ya biashara na Uwekezaji yaliyoanzishwa  na Hayati baba wa Taifa Mwl. JK Nyerere pamoja na Rais wa  zamani wa Iran Mhe. Ayatollah Khamenei , hivyo  katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha uchumi wa nchi unakuwa kwa kasi zaidi, kwa kutangaza bidhaa za Tanzania na kuvutia uwekezaji katika  viwanda vya ndani ya nchi ili kuchochea uzalishaji na kupata masoko ya ndani na nje ya nchi, natoa wito kwa Watanzania kutumia fursa za biashara na Uwekezaji  zilizopo nchini  Iran ili kuongeza mapato kwa Mfanyabiashara mmoja mmoja pamoja na kuchochea uchumi wa  Taifa kwa ujumla .’’ Alisema.

Pia aliongeza kusema kuwa kwa kipindi hiki cha Maonesho tutakuwa na Mikutano ya kuunganisha Wafanyabiashara mbalimbali, tutahakikisha uwekezaji wa sekta ya viwanda unakuwa na unafanikiwa kwa viwango vya juu.


Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TanTrade bw.  Ulingeta O. Mbamba aliongeza kuwa ,Irani kuna fursa za kiutalii, elimu  na kilimo  hivyo tunaweza kuzalisha mazao pamoja  na madini na kupeleka katika soko la  Irani, Pia ni vyema Watanzania wakachamkia fursa ya biashara na uwekezaji zilizopo nchini Iran kwani bidhaa zao zina ubora wa viwango  juu.

‘’Kwa kipindi hiki cha SabaSaba Iran wamekuja kujitangaza  na kuendelea kuunga undugu wa kibiashara na Uwekezaji na  Watanzania  hivyo nawaasa Watanzania waichukulie hii kama fursa ya kujifunza uzalishaji wa bidhaa zenye  ubora viwango vinavyokubalika Kimataifa, pia Irani ni nchi wezeshi kwa Wafanyabiashara wa viwango vya juu vya kati na vya kawaida’’. Alisema.

Pia ameongeza kuwa baada ya Maonesho haya SabaSaba tunategemea kuwa na Maonesho ya Iran na Tanzania ambapo nchi hizo mbili zitaonyesha bidhaa mbalimbali katika sekta ya  kilimo, nafaka, pamoja na elimu. 

Naye Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mhe. Balozi Hussein Alvandi Behineh    Ametoa shukrani kwa  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia TanTrade kwa kupata fursa nzuri ya kushiriki na kuazimisha siku ya Iran katika  Maonesho ya  47 ya SabaSaba na kuitangaza nchi  yao  na bidhaa wanazozalisha.

 ‘Tunatoa wito kwa Watanzania kutembelea Maonesho  ya SabaSaba  na pia kutembelea katika banda letu na kujionea bidhaa tofauti tofauti zenye ubora na viwango vya kimataifa pia waje wajifunze fursa za kibiashara zinazopatika nchini Iran’’ alisema.

Pia aliendelea kusema, Tanzania na Iran inapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja katika biashara ili kuleta uchumi endelevu na wenye Afya pamoja na kujenga Mahusiano mazuri pamoja na kuinuana katika biashara na uwekezaji.