Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

WATANZANIA WASHAURIWA KUTUMIA FURSA ZINAZOPATIKANA KATIKA MAONESHO YA 47 YA DITF KUIMARISHA BIASHARA ZAO.

  • July 25, 2023


........................
Na. Norah Thomas-TanTrade Dar es salaam
5 Julai, 2023.


Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kasim Majaaliwa, Tarehe 5 Julai, 2023 ametoa rai kwa Watanzania kutumia fursa zinazopatikana katika Maonesho ya 47 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam ili  kujifunza na kujipanga kuhudumia masoko makubwa ya ndani pamoja na kuimarisha biashara  za kikanda na kimataifa.

Aidha Waziri Mkuu amesema kufunguka kwa soko huru la Afrika-AfCTFA ambalo linakadiliwa kuwa na walaji zaidi ya bilioni 1.3 kutoka nchi 53 barani Afrika ni fursa kubwa kwa Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Tanzania kutumia nafasi hiyo  ili kujiongezea mapato na kupanua uchumi wa nchi.

‘’ Natoa wito kwa Wafanyabiashara kutembelea Maonesho ya sabasaba  ili kuchangamkia fursa zinazopatikana katika maonesho haya na  kupata  uwezo wa kibiashara na kutumia  vyema fursa zinazopatikana katika masoko na bidhaa za ndani na nje ya nchi’’ alisema.

Ameyasema  hayo  alipokuwa anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika sherehe za Ufunguzi wa  Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya DITF (sabasaba) yanayofanyika katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl. JK Nyerere barabara ya kilwa Dar es salam.


Aidha Waziri Mkuu amezitaka Wizara ya Uwekezaji viwanda na Biashara pamoja na Wizara ya Kilimo zishirikiane kiutendaji katika kuhakikisha wanaandaa  mpango wa pamoja utakaohakikisha uzalishaji unafanyika kulingana na matakwa ya soko la ndani na nje ya nchi.

‘’Wizara hizi mbili lazima zisomane kiutendaji, pia Wataalamu wa TanTrade washirikishwe kikamilifu katika kutekeleza Majukumu ya utafutaji na ufunguaji wa fursa za masoko ya ndani na nje ya nchi,’’ alisema.

Pia  waziri Mkuu ameipongeza Bodi  ya TanTrade ikiongozwa na Mwenyekiti wa bodi  Bw. Ulingeta O. Mbamba kwa kufanya juhudi kubwa   kushirikiana na Wadau mbalimbali katika kuleta mabadiliko  ya Maonesho ya 47  ambayo ni pamoja na  Mapinduzi ya teknolojia,  kuboresha miundombinu na kujenga barabara nzuri za viwango vya rami, hivyo Waziri Mkuu amehaidi kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha  inajenga  mazingira mazuri ya biashara na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Naye Waziri wa Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Shaban Omary amesema, Katika kipindi cha Maonesho ya 46 DITF mwaka 2022  kulipatikana  Mafanikio mbalimbali ambayo ni pamoja na  Makubaliano kumi (10) ya kibiashara ambayo manne (4)  yapo kwenye hatua ya utekelekzaji, kuimarika kwa uwezeshaji wa mazingira ya biashara pamoja na  kuratibu majadiliano ya biashara baina ya nchi na nchi na  uwezeshaji wa wananchi kiuchumi na  kupata masoko ya bidhaa zao.
 ‘’tumeendelea kuweka mkazo mkubwa kwa kuamasisha watanzania kutumia fursa zinazopatikana katika masoko ya nchi mbalimbali ambapo ni pamoja na  kutafuta masoko ya bidhaa za viwanda zinazopatikana na kuzalishwa nchini ili kuongeza pato la taifa.

Akiongezea jambo katika sherehe za uzinduzi huo  naibu waziri wa viwanda amesema Maonesho hayo ni nyenzo Muhimu katika kuwakutanisha Wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi na kuwapa nafasi ya kutengeneza mtandao wa kibiashara pamoja na kupata bidhaa na huduma wanazozalisha.

Naye mwenyekiti wa Bodi ya TanTrade Bw. Ulingeta O. Mbamba amesema Mamlaka hiyo imefanikiwa kushirikiana na Ofisi za Balozi katika nchi ya Kenya na Malawi kuratibu Wafanyabiashara 206 kutoka Tanzania bara na visiwani  katika Misafara ya kibiashara katika nchi ya Malawi ambayo imefanikiwa katika kutangaza fursa kwa Wafanyabiashara wa Tanzania na kujipatia masoko ya bidhaa wanazozalisha.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania (TanTrade)  Bi. Latifa M. Khamis amesema pamoja na majukumu mengine, TanTrade ina jukumu kubwa la kukuza na kuendeleza biashara nchini , hivyo kupitia Maonesho haya TanTrade inatoa wito kwa wadau wote hususani Wafanyabiashara wa ndani kuja kujifunza kutoka kwa wageni namna bora  ya kutumia teknolojia ya kisasa ili kukuza na kuendeleza biashara zao.