Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANZANIA YATUMIA FURSA YA MAADHIMISHO YA SIKU YA KITAIFA YA QATAR KUTANGAZA BIDHAA ZAKE

  • December 18, 2023

18 Desemba, 2023 Doha

Wakati taifa la Qatar likiadhimisha siku ya kitaifa leo tarehe 18 Desemba, 2023, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imetumia fursa ya wingi wa watembeleaji kwenye Maonesho ya Expo2023 Doha kutangaza bidhaa na huduma mbalimbali kutoka Tanzania.

Ikiwa leo ni siku ya mapumziko nchini hapa, watembeleaji wengi wamepata fursa ya kuingia na kujionea bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania, na kupata maelezo ya fursa mbalimbali zilizopo kwenye sekta za Utalii, Kilimo, Biashara na Uwekezaji kutoka Tanzania.
Endelea kufuata (follow) akaunti zetu za Instagram, Twitter, Facebook na Youtube) kwa habari mbali mbali za biashara.