Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANZANIA NI MAHALI SAHIHI PA BIASHARA NA UWEKEZAJI

  • January 14, 2025

14, Januari 2025


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) amewahakikishia Ujumbe kutoka Japani ya kwamba Tanzania ni mahali sahihi pa Biashara na Uwekezajı kupitia kongamano la Biashara na Uwekezajı la Tanzania na Japani lililofanyika leo katika hoteli ya Johari Rotana liyopo jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kigahe ambaye ndiye aliyekua mgeni rasmi katika  Kongamano hilo, ameainisha sekta mbalimbali zenye fursa za uwekezajı kama vile gesi asilia, mafuta, kilimo, na bandari ya Dar es Salaam kwa usafirishaji wa bidhaa mbalimbali  na kutoa wito kwa Wajapani kuchangamkia fursa zinazopatika kwenye sekta ya utalii, na kuwahimiza kutembelea maeneo mbalimbali yenye vivutuo  vya kitalii kama vile Zanzibar, Serengeti, Ngorongoro, Kilimanjaro.