Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

CHAMA CHA WALEMAVU TANZANIA CHATOA TUZO MAALUM KWA TANTRADE

  • July 19, 2024

Dar es Salaam.
Tarehe 19 Julai, 2024.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Latifa M. Khamis leo amepokea tuzo toka Chama cha Walemavu Tanzania ambapo kwa umoja wao wamepongeza TanTrade kwa kutoa fursa kwa wajasiriamali walemavu kila mara kunapokuwa na maonesho.

Bi. Latifa ametoa shukrani kwa CHAWATA kwa tuzo na kuwaahidi kuendelea kuwapa ushirikiano ili kuhakikisha kuwa wanapata masoko ya bidhaa zao.

Aidha Mwenyekiti wa CHAWATA Taifa, Ndugu. Hamadi Abdallah Kumboza ameshukuru TanTrade kwa kuendelea kuwapa ushirikiano na kwa niaba ya Chama ameahidi kuendelea kushiriki katika fursa mbalimbali ambazo zitajitokeza kupitia TanTrade.