TANZANIA YANG'ARA MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA BARANI AFRIKA
- September 8, 2025

7 Sept 2025
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) imeratibu ushiriki wa Taasisi za umma za kimkakati katika sekta ya uwekezaji, Afya na vifaa Tiba, mazingira, ushindani wa biashara, misitu, nishati pamoja na biashara katika maonesho 4 ya IATF 2025 nchini Algeria kunzia tarehe 4 hadi 10 September 2025.
Ushiriki wa Tanzania katika maonesho haya unalenga kuchukua fursa za kibiashara zilizopo katika bara la Afrika ili kupanua wigo wa masoko na kukuza biashara za Tanzania kwa kiwango cha juu ndani ya miaka mitano ijayo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Serera ametembelea Maonesho hayo na kujionea namna ambavyo wadau kutoka mataifa mbalimbali wakitembelea banda na kuingia makubaliano ya kibiashara.
Taasisi nyingine zinazoshiriki maonesho hayo ni pamoja na ZIPA, TASAC, TISEZA, TMDA,PURA, FCC, TFS na NEMC.