TANZANIA NA HARYANA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA KATIKA SEKTA ZA KIMKAKATI, 2025.
- August 11, 2025

Tanzania na Haryana wajadili kuimarisha ushirikiano wa kibiashara katika Sekta za Kimkakati. Sekta hizo ni pamoja na kilimo, Vifaa tiba, viwanda, na teknolojia. MoU mbili katika sekta ya Kilimo na Biashara zilisainiwa kama sehemu ya mafanikio yaliyotokana na kongamano lililofanyika siku ya Haryana India iliyofanyika Katika maonesho ya 49 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, 2025.