Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANZANIA NA DUBAI YAJIPANGA VYEMA KUIMARISHA MIKAKATI KABAMBE YA UKUZAJI BIASHARA

  • December 12, 2024

11, Disemba 2024

-------------

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade ) Bi Latifa M. Khamis, amekutana na ujumbe kutoka Dubai na kuangazia maswala mbalimbali za ukuzaji biashara, namna ya kuwainua na kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu  kwenye sekta ya biashara, walipotembelea ofisi za TanTrade leo tarehe 11 Disemba, 2024 zilizopo katika kiwanja cha JK Nyerere kilichopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Aidha wamepanga kufanikisha ushiriki wa wafanyabiashara wengi zaidi kutoka Dubai kwenye maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba.

 Bi Latifa ameukaribisha ujumbe huo kushiriki Kongamano la Biashara na Uwekezajı la Ziwa Tanganyika linalotarijiwa kufanyika mwanzoni mwa mwaka 2025.