Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI TANZANIA - JAPANI LAZAA MATUNDA.

  • January 14, 2025

14, Januari 2025.

Kongamano la Biashara na Uwekezajı baina ya Tanzania na Japani limefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Johari Rotana, Dar es Salaam likilenga ushirikiano wa kibiashara baina ya nchi hizo mbili kwenye sekta mbalimbali kama  vile Kilimo, Bima, Uzalishaji wa Viwanda, Ujenzi, Usafirishaji, Tekinolojia ya Mawasiliano nk.

Aidha kongamano hili baina ya Tanzania na Japani limelenga kuhimarisha uhusiano wa kibiashara kuelekea Maonesho makubwa zaidi ya Biashara duniani EXPO2025 Osaka, Kansai Japan. TanTrade inaratibu mchakato mzima wa kushiriki Expo2025.