Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE ,BODI YA NYAMA KUJA NA MAONESHO YA PAMOJA YA BIDHAA YA NYAMA

  • November 29, 2023

28 Novemba, 2023

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imekutana na kufanya kikao na Bodi ya Nyama Tanzania  (TMB) na kupanga mikakati ya kuwa na maonesho ya pamoja ya kutangaza bidhaa ya nyama, fursa na elimu ya nyama.

Kikao hicho  kimefanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Bodi hiyo ambapo TanTrade  iliwakilishwa na Maafisa Biashara ambao ni Mohamed Tajiri,  Eliabu  Lwabyago, Boniface Mrema, Dorothy Makumba  Samira Mohamed na Marcelina Shirima.