Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAENDESHA MAFUNZO YA AWALI KWA WAONESHAJI

  • June 30, 2024

27/06/2024
Dar es salaam

Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania, TanTrade imeendesha semina ya awali kwa waoneshaji kabla ya maonesho yatakayoanza tarehe 28 Juni, hadi tarehe 13 Julai, 2024 iliyofunguliwa na Bw. Crispin Mathew Luanda ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Biashara kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi Latifa M Khamis ilyofanyika katika ukumi wa Dome uliopo katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Aidha Bw. Luanda ameeleza kuwa semina hii ni mahususi kwa kutoa maelekezo kwa waoneshaji juu ya kanuni za ushiriki katika monesho ya Sabasaba mwaka 2024, ulinzi na usalama wakati wa maonesho, athari za kiafya zinazoweza kujitokeza kipindi cha maonesho na jinsi ya kujikinga, zoezi la kuchagua banda bora pamoja na taratibu za kuomba visa na masuala ya vibali kwa wageni wanaotoka nchi za nje.