BARAZA LA WAFANYAKAZI TANTRADE KATIKA UKUZAJI WA BIASHARA
- March 12, 2025

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi Latifa M. Khamis ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi ametoa rai kwa watumishi kutumia vipaji na utaalamu katika kushauri na kutekeleza majukumu ili kufikia malengo ya kukuza biashara wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi cha kujadili masuala mbalimbali ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi likichofanyika leo tarehe 12 Machi, 2025 katika Ofisi za TanTrade zilizopo kiwanja cha Mwl. JK Nyerere, barabara ya Kilwa, Jijini Dar es Salaam.