Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YABORESHA MABANDA KWA AJILI YA MAONESHO YA 47 YA DITF - SABASABA 2023

  • July 21, 2023



.................................
Na. Norah Thomas-TanTrade Dar es salaam.
12 Juni, 2023.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade @tantradetz imejipanga kufanya Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Dar es salaam(Saba Saba) ya Mwaka 2023 kuwa ya kupendeza na kutatua changamoto za kibiashara ambapo ni pamoja na kuwakutanisha wadau wa biashara kutoka nje na ndani ya nchi.   Hayo yamefanyika baada ya TanTrade kufanya maboresho ya  Mabanda yake pamoja na kutatua changamoto zilizojitokeza katika Maonesho ya Miaka iliyopita.

Akizungumza hayo katibu wa Kamati ya Ukodishaji Mabanda (SAC), ndugu Baraka Peter amesema kwamba kwa mwaka huu Maonesho yamepangwa kuwa ya namna yake kwani Mamlaka imeboresha mabanda yake pamoja na Miundombinu mingine ya Maonesho hayo ya kimataifa.

Pia amesema kuwa zoezi la uandikishaji wa Washiriiki katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara Dar es salaam (SabaSaba) linaelekea ukingoni, Hivyo ni muhimu kwa Washiriki waliojiandikisha kukamilisha ada ya ushiriki.
’Napenda kuwakaribisha Washiriki wote kwa ajili ya kujaza fomu za Mabanda na kutembelea katika tovuti ya TanTrade ambayo ni www.tantrade.go.tz ili kuwasilisha taarifa za Washiriki kwa ajili ya kuchukua vitambulisho mapema’’Alisema.
Maonesho ya Sabasaba yanatarajiwa kuanza Tarehe 28Juni hadi Tarehe 13 Julai 2023