TANTRADE KUKUZA UHUSIANO WA KIBIASHARA BAINA YA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI
- August 15, 2025

14 AGOSTI, 2025.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imekutana na ujumbe kutoka Afrika Kusini na kuangazia mipango madhubuti ya kuendeleza ushirikiano wa kibiashara baina ya nchi hizo mbili.
Aidha ujumbe huo kutoka Afrika Kusini umetembelea ofisi za TanTrade kwa lengo la kujifunza maswala na miongozo mbalimbali ya kuleta mapinduzi ya kibiashara kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi na Mataifa hayo kwa ujumla. Biashara kubwa baina ya nchi hizo mbili ni pamoja na dhahabu, mbao, maua, Apples, maharage ya soya, nyama, tambi, mvinyo, viungo(spices), vifaa vya Ujenzi kama vile mabati, misumali, tarazo, bidhaa za ngozi, nk. Mazungumzo hayo ya kibiashara yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi za TanTrade zilizopo katika Uwanja wa Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.