TANTRADE YAFANIKISHA USHIRIKI WA WAFANYABIASHARA KUTOKA TANZANIA NCHINI BRAZIL
- April 29, 2024

29 Aprili 2024
Sao Paul, Brazil
Mmlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Brazil imefanikiwa kuratibu maonesho ya Brazil Agri Show 2024, ambayo yamelenga katika kuwatafutia masoko wafanyabiashara wa Tanzania nchini Brazil katika sekta ya Kilimo, Vipuri na Matairi, Umwagiliaji, Fedha, Mbolea na Dawa za kuulia wadudu, Mashine za kilimo pamoja na Mbegu.
Aidha kati ya nchi 20 toka Afrika, wafanyabiashara wawili kutoka Tanzania ambao ni Major Peter na Mohinder Singh Rahel wamepata fursa ya kufanya biashara na wanunuzi wakubwa toka Brazil.
Maonesho haya yanayofanyika katika jiji la Sao Paul yameanza leo tar 29 April hadi tar 3 Mei na yamefanikiwa kuvutia zaidi ya wanunuzi 800 na watembeleaji 190,000.