Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA UBUNIFU SEKTA YA UMMA

  • December 17, 2025

16 Disemba, 2025

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeshiriki na kushinda tuzo ya Ubora katika Uhamasishaji Biashara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Uchumi. Tuzo hizo za sekta ya Umma zinaangazia ubunifu unaofanywa na taasisi mbalimbali za umma kwa muktadha wa kutoa huduma bora zinazoakisi maendeleo endelevu ya uchumi wa Tanzania. TanTrade imekua ikifanikisha hayo kupitia Maonesho ya Sabasaba, kuratibu Maonesho mbalimbali ya Kimataifa kama vile Expo's, Mifumo mbalimbali ya Kidigitali ya Biashara kama vile Trade Portal, Biashara App, nk. Hafla ya tuzo hizo zimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.