TANTRADE YATOA MAFUNZO KWA WAFANYABIASHARA KUTOKA MKOA WA DAR ES SALAAM
- September 17, 2025

16 September, 2025
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imetoa mafunzo ya usimamizi wa biashara kwa wajasiriamali na wafanyabiashara waliokusanyika kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam lengo likiwa ni kuwajengea uwezo katika kukuza na kuendeleza biashara, kufanya tafiti za biashara zao, kutoa huduma bora kwa wateja na kushughulikia malalamiko ya wateja kwa haraka.
Aidha,TanTrade imewasisitiza wafanyabiashara kuzalisha bidhaa bora na kufanya ubunifu ili ziweze kushindana kibiashara ndani na nje ya Tanzania. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro katika viwanja vya Mwl J.K.Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.