Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YASHIRIKIANA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE KUTOA MAFUNZO YA UUZAJI BIDHAA, UINGEREZA.

  • March 28, 2024

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTARADE) kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Viwanda na Biashara Imeratibu Semina ya Wafanyabiashara kuhusu fursa ya kuuza bidhaa katika soko la Uingereza kupitia Mpango wa Biashara wa Uingereza na Nchi zinazoendelea (UK-DCTS)

Semina hii ya inayofanyika katika ukumbi wa JNICC ulipo Jijin Dar es salaam. Inalenga kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na nchini Uingereza ili kujenga uwezo wa taratibu na vigezo na hivyo kuwafungulia fursa za Masoko zinazopatikana nchini Uingereza
                                                            Wakimwakilisha Mkurugenzi Mkuu TANTRADE Bi. Latifa M. Khamis, Meneja Uhusiano kwa Umma na Masoko Lucy Mbogoro pamoja na Afisa Biashara (Masoko ya Ndani na Nje ya Nchi) Bw. Deo Shayo wameshiriki Semina hii ambayo imefunguliwa rasmi na Mhe. Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Ashatu Kijaji.

Ushiriki wa TANTRADE kama Taasisi yenye Mamlaka ya kusimamia, kukuza na kutangaza Masuala ya Biashara Ndani na Nje ya Nchi katika semina hii utaleta faida kubwa kwa wafanyabiashara watakaotumia fursa hii.

Aidha, TanTrade inaalika wafanyabiashara kuendelea kujengewa uwezo, kupata taarifa na kushiriki shughuli za ukuzaji masoko ikiwemo Sabasaba ambapo tayari maandalizi yameanza