Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YASHIRIKIANA NA TAWEN KUWAJENGEA UWEZO WAJASILIAMALI WANAWAKE TANZANIA.

  • July 21, 2023



Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade) mapema leo imeshirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Women Empowerment Network (TAWEN)  kutoa semina ya Mafunzo ya ujasiliamali kwa Wajasiliamali Wanawake zaidi ya 500  iliyofanyika katika ukumbi wa SabaSaba ndani ya  Uwanja wa Mwl, JK Nyerere barabara ya Kilwa Dar es salaam.

Akiongea katika Semina hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa shirika ilo bi. Florence Masunga  amesema kuwa nia ya TAWEN ni kuwawezesha wanawake kiuchumi, kiutamaduni na kuwatafutia fursa mbalimbali za  masoko ya bidhaa zao zinazopatikana ndani na nje ya Tanzania.

‘’Tumeshirikiana na  wawezeshaji mbalimbali  kama vile TanTrade na wengine wengi ili kuwasaidia wanawake  kuzitambua fursa za kibiashara zinazopatikana nchini, pamoja na kuwafundisha namna bora ya uzalishaji wa  bidhaa zinazokidhi viwango vya kimataifa’’, alisema.

Pia aliongeza kuwa,
‘’Mwaka jana kwa kushirikiana  na TanTrade tuliandaa Mkutano mkubwa  wa Wajasiliamali Wanawake zaidi ya 1000 katika hotel ya Mount Meru jijini Arusha na kuwapa semina ya kuwawezesha na kuwajengea uwezo wanawake hao pamoja na kuboresha biashara na shughuli zao’’.

Pia alisisitiza kuwa wanawake wanaweza kujenga Tanzania  ya tofauti zaidi ya inavyoonekana kwani wanawake ndio chachu ya kuleta maendeleo katika jamii.

Nae afisa biashara kutoka Tantrade bi Eliza Haule alielezea kuwa Kupitia mkutano huu utasaidia kujenga fursa kubwa kwa wanawake na kuwainua kiuchumi.