Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YASHIRIKIANA NA CTI KATIKA UFUNGUZI WA MAONESHO YA TIMEXPO 2023

  • October 5, 2023

4 OKTOBA, 2023
DAR ES SALAAM.



Mamlaka ya Maendeleo na Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kushirikiana na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (Confederation of Tanzania Industries - CTI) leo tarehe 4 Oktoba, 2023, wamefungua rasmi Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Viwanda Tanzania (TIMEXPO ) yanayofanyika kwa muda siku tatu kuanzia tarehe 4-6 Oktoba, 2023 katika moja ya kumbi  maaarufu ya  Aga Khan Diamond Jubilee Hall- Jijini Dar es salaam, tarehe 4 Oktoba 2023.


Kupitia sherehe za ufunguzi wa Maonesho hayo, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Faustine Mkenda ametoa pongezi kwa taasisi zilizo toa ushirikiano wa uratibu ikiwemo TanTrade kwa kufanikisha na kuboresha Maonesho hayo kuwa katika kiwango cha kimataifa. Pia, pongezi zingine zimeenda kwa watengenezaji wa bidhaa kwani wameonesha ubunifu mkubwa ambao utaleta mafanikio makubwa katika soko la biashara na kuonesha fursa mbalimbali kuzingatia sheria zilizopo ili kudumisha uhusiano mzuri wa maendeleo makubwa ya kiuchumi ndani na nje ya nchi.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TanTrade Prof. Ulingeta .O. L Mbamba amesema Maonesho hayo ya TIMEXPO ni kichocheo cha ufumbuzi wa maendeleo ya viwanda kutokana na maendeleo ya kiteknolojia yanayoendelea. Pia, ametoa shukrani za dhati kwa Waheshimiwa, Mabalozi na  Wafanyabiashara wote waliohudhuria Maoneshobhayo ambayo yatakuwa chachu ya maendeleo ya viwanda na  mafanikio hasa kiuchumi ndani na nje ya nchi.