Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YASHIRIKI KIKAO KAZI CHA KITUO JUMUISHI CHA FORODHA CHA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

  • September 29, 2023

Tarehe 28 Septemba, 2023.
Nairobi.
 
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inashiriki  kikao Kazi cha mwongozo wa Kituo Jumuishi cha Forodha (  EAC One Stop Boarder Point - OSBP ) Jijini Nairobi nchini Kenya.

Lengo kuu la kikao ni kupitia na kuridhia  OSBP procedure Manual ambayo inalenga Kurahisisha Mazingira ya Ufanyaji wa Biashara kwa nchi za Afrika Mashariki hususani Mipakani.

Kituo Jumuishi cha Forodha Mipakani kitarahisisha biashara ambapo Wafanyabiashara  hawatalazimika kusimama na kukaguliwa pande mbili za Nchi zinazopakana na badala yake ,watasimama upande mmoja tu wa nchi wanayopeleka bidhaa zao na Ukaguzi kufanyika mara Moja Kutoka kwa Maafisa wa Forodha wa Nchi zote mbili.Hatua hiyo itasaidia kuondoa Urasimu Mipakani na kupunguza Muda wa Wafanyabiashara kukaa kwenye Foleni Mpakani.

Nchi zinazounda EAC ni Tanzania,Kenya,Uganda, Sudani Kusini,Rwanda, Burundi na Kongo DRC.

Kikao hicho cha siku mbili  kinatarajiwa kuja na Maboresho Makubwa ya kiutendaji Mipakani baada ya Maridhiano kadhaa katika uendeshaji  kwa lengo la kupunguza ama kuondoa kabisa usumbufu kwa wafanyabiashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na hivyo kukuza Biashara Miongoni mwa nchi wanachama.Hatua hiyo inafikiwa baada ya mchakato wa Muda mrefu Tangu mwaka 1996 lilipotolewa wazo la kuanzishwa kwa vituo Jumuishi vya Forodha Mipakani kwa nchi za Afrika Mashariki ( EAC)  na   baadaye mwaka 2021 kuingiwa Makubaliano ya awali na hatimaye utekelezaji na uboreshaji wa Maeneo yenye  changamoto unaendelea Jijini Nairobi Kenya.Kukamilika kwa Maboresho kuna tija kubwa sana kwa Jumuiya ya wafanyabiashara nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa Ujumla.