Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YASHIRIKI MKUTANO WA UTATUZI WA VIKWAZO VYA KIBIASHARA ULIOPO MIPAKANI BAINA YA TANZANIA NA ZAMBIA

  • April 23, 2024

TanTrade imeshiriki Mkutano wa Pili wa Pamoja kujadili changamoto za Biashara kati ya Tanzania na Zambia, Mkutano huo umekutanisha makatibu wa kuu wa nchi zote mbili ambao ulioanyika katika mpaka wa Tunduma Tanzania tarehe 17 Aprili 2024.

Katika Mkutano upande wa Tanzania katibu Mkuu wa Wizara na Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na katibu mkuu wa Wizara ya Biashara n Viwanda wa Zambia Bi Lilian Bwalya pamoja na Katibu mkuu wa Uchukuzi Pro. Godius Kayharara waliongoza mkutano huo wenye lengo la kutatua kero za vizuizi 33 vilivyokuwepo katika boda ya Zambia ambapo kupitia kikao hicho kero nyingi zimetatuliwa hadi kufikia kero 11.

Aidha awali Tanzania ilikuwa na kero 15 kabla ya kuingia kwenye majaridiliano hayo ambapo takribani kero Nne ziliweza kutatuliwa ilikurahisisha michato ya kibiashara.