Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YASHIRIKI MAANDALIZI YA EXPO OSAKA 2025, JAPAN

  • November 14, 2023

TANTRADE YASHIRIKI MAANDALIZI YA EXPO OSAKA 2025, JAPAN
_______
14 Novemba, 2023
 Osaka- Japan.

Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa M.Khamis ameungana na Balozi wa Tanzania Nchini Japan Mhe Baraka M. luvanda na Viongozi wengine wa nchi mbalimbali kushiriki siku ya kwanza ya mkutano wa 3 wa Kimataifa wa nchi washiriki wa Expo 2025 Osaka /Japan .

Washiriki wa Mikutano hii ni Taasisi za  ukuzaji Biashara (Trade Promotions-TPOs) Duniani ambazo  zinatoka Nchi wanachama wa Shirikisho la Maonesho ya Biashara Duniani ( Bureau for International Exhibitions-BIE) zikiwakilisha nchi zao ambapo Jumla ya TPOs 501 zimeshiriki  mkutano huu  utakaoendelea kwa muda wa siku 3.

Tanzania inatarajiwa kutumia fursa za Maonesho haya makubwa mwaka 2025 kujitangaza kwa kuonesha bidhaa za Kimkakati, kuunganisha uzalishaji na masoko na kutangaza vivutio na fursa za Uwekezaji ili kukuza Biashara na Uchumi wa Taifa.