Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YASHIRIKI UZINDUZI WA RIPOTI YA STANBIC BANK AFRICA YA TAFITI ZA BIASHARA 2023

  • November 24, 2023

23/11/2023
Dar es salaam.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeshiriki katika uzinduzi wa Ripoti ya tathmini ya Hali ya Biashara kupitia Stanbic Africa katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, Dar es Salaam, kufuatia utafiti uliofanyika
ambao ulihusisha biashara 2500 katika nchi 10 za Afrika na kampuni 227 nchini Tanzania, kati ya hizo 70% ilikuwa biashara ndogo, 17% biashara kubwa na 13% ni Makampuni yaliyofanyika Dar, Mwanza, Arusha, Moshi na Mbeya.

## Matokeo ya utafiti yanaashiria umuhimu wa biashara ndogo ndogo na uhitaji wa wadau kushirikiana ili kukuza biashara nyingi ziweze  kuingia katika masoko na mauzo ya nje. Taasisi za fedha zitatarajiwa kutoa mikopo zaidi inayoendana na mazingira ya uchumi wa Tanzania ili kuongeza kasi ya miamala na biashara thabiti itakayo vutia biashara na uwekezaji zaidi;

## Ripoti imeonyesha kupungua kwa 1% ya mkopo inayochululiwa katika Sekta ya Biashara kwa kipindi cha Septemba.2022-Mei 2023, huku wafanyabiashara wakiona upatikanaji wa mikopo kuwa mgumu zaidi licha ya sera thabiti za fedha zilizopo. Hii inaleta hitaji la kufanya mikopo kuwa muhimu zaidi na kutengenezwa mahususi  kwa bidhaa kimkakati/sekta maalum kama vile kilimo kwa kuzingatia kuweka gharama za chini za kukopa (viwango vya riba)

## TanTrade imebainisha uzoefu kwa wafanyabiashara wengi wadogo ambao ni wakulima au wanaojishughulisha na mazao ya kilimo ambao  hulalamika kwamba mikopo ya benki nchini haijatengenezewa kwa kuzingatia mahitaji yao kwa mfano mkopo kwa ajili ya kilimo na shughuli zinazohusiana na hizo ambazo ni za msimu kuwa na viwango sawa na wale wanaokopa ili tu kununua bidhaa na kuuza papo kwa hapo ( merchandise)

## kuongezeka uelewa  uliopo wa Masoko ya AfCFTA  na masoko mengine miongoni mwa makampuni kutoka 22% mwaka 2022 hadi 40% mwaka 2023. Ripoti imeonesha kuelimisha na kujenga uelewa kuhusu AfCFTA miongoni mwa kampuni kumeanza kuzaa matunda. Aidha, kwa upande wa TanTrade,  timu ya wataalam ilitumwa kwa kampuni katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ikiwemo Mbeya ambako fursa kuhusu AfCFTA ziliwasilishwa na hivyo kupongezwa kwa jitihada hizo;

#Wadau kutoka sekta ya umma na binafsi, taasisi za fedha walitoa hoja ya kuendelea kuungana na TanTrade kwa kuunga mkono kampeni yake ya wataalam katika Kujenga uwezo na program atamizi ili  biashara ziweze kufaidika na AfCFTA.
## Ripoti hiyo inaonesha kuwa Biashara ya mipakani inaimarika kwa kiasi kikubwa kati ya Tanzania na nchi mbalimbali hasa China na Kenya kutokana na mipango ya pamoja katika kutangaza bidhaa za Tanzania. Kwa mfano hivi sasa (Nov. 2023) maonyesho ya China Import-Export Expo (CIEE) ambapo Tanzania imeonyesha sampuli za bidhaa za Tanzania zikiwemo Chai na Kahawa.

## Migongo iliyowekwa pia ilitambuliwa kuwa
Upatikanaji wa data; changamoto ambayo imeangaziwa sio tu Tanzania bali nchi nyingi za Afrika. Takwimu zisizohakika na zisizotabirika pia kuathiri majaribio ya kuendeleza na kukuza biashara; hususan wakati fursa zinapotokea wazalishaji hushindwa kuhudumia kutokana na pengo la taarifa. vikwazo  vingine vimeelezwa kuwa vya kiushuru( Tariffa) na vizuizi visivyo vya ushuru( Non Tarrifs) na pamoja na miundombinu ya usafirishaji.

 ## Kwa ujumla, Stanbic Bank Africa Trade Barometer imeonesha na kutia moyo kuwa kuna kuimarika kwa hali ya Biashara ya Tanzania katika kipindi cha miaka miwili iliyopita katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kutokana na sera za biashara nzuri za kukuza biashara. Aidha, biashara nyingi zilizofanyiwa utafiti (94%) zinatarajia ongezeko la mapato katika mwaka ujao (2024); kutokana na ongezeko linalotarajiwa la mahitaji ya bidhaa na huduma. Hii pia inaashiria mitazamo chanya juu ya jukumu ambalo serikali inatekeleza kusaidia shughuli za biashara.Inasisitiza ushirikiano wa hali ya juu kati ya wahusika wakuu wa biashara na washikadau kupewa kipaumbele.

## Benki ya Stanbic yaahidi kufanya kazi na TanTrade kupitia MoU iliyopo ili kujenga uwezo wa Tanzania Enterprises katika masoko.