Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI (MEI MOSI 2023) DAR ES SALAAM.

  • July 21, 2023

........................

Na. Norah Thomas-TanTrade Dar es salaam.

Watumishi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) wameshiriki Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika Jiji la Dar es salaam.

Maadhimisho hayo hufanyika kila Mwaka ambapo Mwaka huu kitaifa yamefanyika mkoani Morogoro yakiambatana na kauli mbiu isemayo “Mishahara bora na ajira za staha ni nguzo kwa Maendeleo ya Wafanyakazi ”
Aidha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia  Hassan Suluhu amesema kuwa nyongeza ya mshahara ya kila mwaka kwa Watumishi wa Umma ambayo ilikua imesimama kwa muda mrefu itaanza kuzingatiwa mwaka wa fedha 2023/ 24 na kuendelea kwa miaka ijayo.

Mhe. Samia amesema hayo Mei Mosi 2023, mkoani Morogoro wakati akihutubia katika siku hiyo ya wafanyakazi iliyoadhimishwa Kitaifa mkaoni hapo.

"Nawahakikishia kuwa, katika uongozi wangu Madaraja yataendelea kupanda, mafao ya wastaafu yatalipwa kwa wakati, kubadilisha kada itazingatiwa na waliondolewa kazini wataendelea kulipwa stahiki zao", amesisitiza Mhe. Samia.

Ameongeza kuwa, Serikali inaendelea kulipa madai ya wafanyakazi baada ya kumaliza uchambuzi wa madai hayo.