TANTRADE YASHIRIKI MKUTANO WA 9 WA FURSA ZA USAFIRISHAJI NA MIUNDOMBINU AFRIKA MASHARIKI 2023
- December 15, 2023

Dar es salaam
13 Desemba, 2023
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeshiriki Mkutano ulioanza tarehe 11 hadi 12 Desemba 2023 uliofanyika katika Hoteli ya Four Points Dsm, kujadili fursa katika sekta ya Usafirishaji na Miundombinu Afrika Mashariki. Mkutano huo ulioratibiwa na Taasisi ya Bricsa Consulting kwa kushirikiana na Wizara ya Uchukuzi na Washiriki wa kikanda na Kimataifa.
## Aidha, katika wasilisho la Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ( DART) na pia Shirika la Reli ( TRC) ilibainishwa namna miundombinu yake inavyofungamanishwa (TOD) na sekta muhimu za kibiashara ili kukuza Uchumi jumuishi. Maeneo muhimu ambayoni pamoja na uwanja wa Maonesho wa Sabasaba Dar es salaam ( Mwl. Nyerere Trade Fair Ground) unaomilikiwa na TanTrade-kurasini, Kituo cha Biashara za Kimataifa cha Afrika Mashariki- Ubungo( EACLC) na pia Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam (JNIA) yamebainishwa kuwa miongoni mwa maeneo ya Kimkakati katika miradi kibiashara inayofungamanishwa na miundombinu ya kisasa ya usafirishaji.
## Teknolojia muhimu za usafirishaji zilizojadikiwa ni pamoja ongezeko la pikipiki na magari yanayotumia umeme na gesi, magari ya angani (cable cars), kamera za usimamizi wa barabarani(smart Traffic Management)na Express way ( Road toll).
## Baadhi ya Fursa zilizotangazwa katika maeneo mbalimbali ni pamoja na viwanja vya ndege 59 vinavyoasimamiwa na Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA), uwekezaji Express-way (Kibaha Chalinze, Chalinze Morogoro na pia njia nne kutoka Morogoro- Dodoma) kupitia TanRoads, Bandari ya Kwala, Reli ya Kisasa SGR, uwekezaji wa Viwanja vya ndege maeneo mbalimbali Zanzibar.
## TanTrade inaendelea kuwa mbia muhimu wa kushauri mtangamano wa miundombinu ya usafirishaji na Masoko katika sekta mbalimbali kwa kuzingatia nafasi yake katika uendelezaji na ukuzaji wa Biashara ndani na nje ya nchi.