Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YASHIRIKI KURATIBU KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI, MRADI WA SGR

  • March 5, 2024

05 Machi 2024
Mwanza.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na Rais, Dr. Samia Suluhu Hassan imefanya uwekezaji mkubwa kwenye Sekta ya Usafirishaji moja ya uwekezaji huo ikiwa ni Reli ya Kisasa (SGR).

Kwa kutambua umuhimu wa Reli hii, Tanzania Railway Corporation (TRC) imefanya kongamano la Biashara na uwekezaji ambalo linakutanisha pamoja wadau kutoka Taasisi za Umma na sekta binafsi.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria kwenye kongamano hili ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi. Latifa Khamis. Mkurugenzi Mkuu MSCL Mr. Eric Hamissi, Mkurugenzi Mkuu LATRA CPA Habibu Suluo na Mkurugenzi Mkuu TRC Masanja Kodogosa.
Kongamano hili limejikita katika kuangalia fursa zinazopatikana pembezoni mwa reli hii ya kisasa ambazo zitachangia maendeleo katika Biashara na uwekezaji.

Katika kuunganisha nguvu kwenye eneo hili Serikali ya Tanzania kupitia TanTrade na Nchi ya Iran walikutana nakufanya kongamano la biashara mwezi Februari 2024, na sasa nchi hizi zinategemea kufanya biashara ambayo itahusisha kusafirisha bidhaa kutoka Tanzania kwenda Iran hivyo kukuza mahusiano ya kibiashara na uchumi wa Tanzania.

Kikao hiki pia kimebainisha jinsi ambavyo wafanyabiashara na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi watakavyonufaika baada ya uendeshaji kuanza.