Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

Uchaguzi tarehe 29 Oktoba, 2025

Kura yako haki yako, jitokeze kupiga kura

Uchaguzi 2025

TANTRADE YASHIRIKI KONGAMANO LA WAFANYABIASHARA KUTOKA OMAN.

  • September 9, 2025

8 SEPTEMBA 2025.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade katika kutekeleza moja ya jukumu lake la kuendeleza Biashara za Tanzania, leo imeshiriki kongamano la biashara baina na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ujumbe wa Chemba ya Wafanyabiashara kutoka Oman. Nchi hizo mbili zimeangazia fursa mbalimbali za kibiashara kwa bidhaa mbalimbali kutoka sekta ya Kilimo, Umeme na Mafuta. Kwa upande wa Tanzania imewaakikishia wageni hao kuwa Tanzania inasimamia mazingira rafiki ya Kibiashara na uwekezajı kwa kuzingatia punguzo kubwa la kodi kwa kulinganisha na nchi nyiginezo Afrika.

Aidha ujumbe kutoka Serikali Omani imepongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwapokea vyema na kuwafungulia milango ya Biashara na Uwekezajı, kubadilishana maarifa ya kibiashara. Uhusiano wa Biashara na Uwekezajı baina nchi hizo mbili umekua  imara kwa miaka ishirini kwa Dira ya Maendeleo ya Tanzania ya 2050 na ya  Omani ikiwa ni 2040.