Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YASHIRIKI KATIKA MKUTANO WA ANA KWA ANA (B2B) KATI YA TANZANIA NA UTURUKI

  • June 5, 2024

4/06/2024.
Dar es salaam


Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara(TanTrade) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Uturuki wameratibu Mkutano wa biashara wa ana kwa ana kati ya Tanzania na Uturuki ambao umefanyika leo katika ukumbi wa Johari Rotana jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika Mkutano huo Mkurungezi Mkuu wa TanTrade Bi Latifa M. Khamis alitumia fursa hiyo kuainisha fursa za bishara zilizopo Tanzania na kuwaalika wadau katika Maonesho ya Kimataifa ya biashara ya Dar es salaam maarufu kama SabaSaba yanayotarajia kuanza mwishoni wa mwezi huu wa sita.

Mkutano huo umehudhuriwa na taasisi mbalimbali , zikiwepo sekta za Umma, binafsi pamoja na wafanyabiashara kutoka Tanzania wamekutana na wafanyabiashara wa kutoka Uturuki kwa lengo la kubadilishana fursa za kibiashara na uwekezaji ambazo zinapatikana baina za nchi hizi mbili.