Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YARATIBU KLINIKI YA BIASHARA KATIKA VIWANJA VYA BUNGE

  • May 22, 2024

21/05/2024
Dodoma.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade kwa kushirikiana na taasisi wezeshi zimeratibu Kliniki ya Biashara katika Maonesho ya Wiki ya Viwanda na Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Bunge Dodoma.
                                                                                                                                                                                  Lengo la kliniki hiyo ni kusaidia ukuaji endelevu na kuimarisha mazingira wezeshi ya biashara nchini kwa kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya biashara nchini ambazo zinachangia kuongeza gharama za ufanyaji wa biashara (Cost of doing business) na hivyo kuwa kikwazo kikubwa katika ukuaji wa biashara nchini hususani biashara ndogo na za kati.

Aidha Viongozi na Wabunge mbalimbali waliweza kuhudhulia kliniki hiyo na kuipongeza TanTrade kwa kuratibu Kliniki hiyo ya Biashara yenye lengo la kutatua kero za wafanyabiashara

Viongozi hao walizielekeza Taasisi hizo zikiongozwa na TanTrade kuhakikisha  wanawafikia wafanyabiashara wengi zaidi kwa kutembelea mikoa ya Tanzania Bara na visiwa vya Zanzibar wakati wa vikao vya Bunge la Zanzibar.

Utoaji wa Elimu ya Biashara ni pamoja nakuendesha baadhi ya kliniki za biashara ambapo ni jukumu moja wapo la Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).