TANTRADE YAKUTANA NA KAMPUNI YA CCPIT TOKA CHINA
- May 17, 2024

Dar es Salaam,
15 Mei, 2014
Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa M. Khamis leo amepokea ujumbe kutoka Kampuni ya CCPIT yenye makazi yake jimbo la Hunan, China.
Kampuni hii inayojishughulisha na ukuzaji Biashara na Uwekezaji imefanya ziara nchini kwa lengo la kukutana na wafanya biashara wa Kitanzania katika sekta za usindikaji na teknolojia ya kilimo.
Bi. Latifa ameelezea jinsi ambavyo TanTrade imekuwa ikishirikiana na China kupitia Kampuni na taasisi mbalimbali ambazo hushiriki katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam (DITF) na kuongeza kuwa Mamlaka inashukuru Serikali ya China kwa kuweka kipaumbele katika kukuza Biashara kati ya Tanzania na China kwa kuhamasisha wafanyabiashara wa China kushiriki katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam ambayo yanategemewa kuwa yenye utofauti mkubwa hasa katika eneo la teknolojia za uzalishaji bidhaa ambazo China wanategemea kuleta nchini.