Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAKUTANA NA UJUMBE WA SERIKALI YA JIMBO LA SHANDONG

  • November 10, 2023

Novemba 10, 2023
 Shanghai China

Ujumbe toka Serikalini Jimbo la Shandong ambao waliongozana na wajumbe toka chama cha  CPC (COMMUNIST PARTY OF CHINA), TanTrade  na EACLC walikutana katika Ofisi za East Africa Commercial and Logistics Centre (EACLC) zilizopo jijini Shanghai, China.

Madhumuni ya kikao hicho ni wito wa TanTrade kuonesha fursa za biashara na uwekezaji  zilizopo nchini Tanzania.

Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa TanTrade Bw Fortunatus Mhambe aliwaeleza Urafiki wa Tanzania na China ambapo mwaka 1971 Dkt. Salim Ahmed Salim alisaidia China kupata kura za nchi 30 barani Afrika na hivyo kupata Kiti cha Kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Aidha   Bw. Mhambe alielezea mazingira bora ya uwekezaji na biashara ikiwamo hali ya utulivu na usalama na fursa mbalimbali zilizopo katika Sekta ya Utalii, Kilimo, Mafuta na Gesi, Madini, bidhaa na mazao mbalimbali.

Vilevile ujumbe huo ulihitaji kupata taarifa ya hali ya Maendeleo ya Viwanda nchini Tanzania na kuona maeneo ambayo China inaweza saidia katika eneo la Teknolojia na mafunzo.

Aidha, ujumbe huo pia ulihitaji kupata taarifa kuhusu sekta ya Madini Tanzania hususani taratibu za ununuzi na uwekezaji katika madini ya dhahabu.

Pia ujumbe huo ulionesha nia ya kufanya kilimo cha pamoja cha shamba matunda.

Ujumbe huo vilevile umesema unapanga kutembelea nchini Tanzania ukiwa na ujumbe wa watu wasiopungua 100 mwezi Machi na Aprili,  2024 kwa nia ya kutembelea
Viwanda vidogo, vya kati na vikubwa na
kuziona baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa Tanzania.

Na mwisho muwakilishi wa ujumbe huo alisema kuwa jimbo lao limedhamiria kuandaa warsha kubwa itayokuwa na wawekezaji wakubwa wenye nia ya kuja kuwekeza Tanzania na kuahidi kualika ujumbe (Delegation) kutoka Tanzania kushiriki katika warsha hiyo na kupewa nafasi ya kuzielezea fursa zilizopo nchini Tanzania kwa upana wake ambapo warsha itafanyika Mwezi  Desemba, 2023.

Kwa upande wa TanTrade, Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa Biashara, Bw. Mhambe aliendelea kuwahakikishia juu ya usalama wa wawekezaji Tanzania na kwamba Tanzania siku zote huwalinda wawekezaji wote.

Aidha, Bw. Mhambe aliwakumbusha wajumbe mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM)  na  CPC tokea wakati wa Hayati Mwl. Julius Nyerere na aliyekuwa muasisi na  kiongozi wa Taifa la China Mao Zedong.

Aidha,  Mhambe aliongeza kwa kusema kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya TanTrade na Kampuni ya EACLC, TanTrade illifikia makubalino ya kuwapa nafasi ya kuleta washiriki wa Maonesho makubwa ya Dar es Salaam International Trade Fair (DITF).

Mwisho Bw. Mhambe aliwakaribisha wajumbe (Wawekezaji) hao kushiriki katika Maonesho yajayo ya 48 ya DITF, 2024.