Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAKUTANA NA UJUMBE TOKA CHINA

  • May 15, 2024

14 Mei 2024,
Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa M. Khamis amepokea  ujumbe kutoka China ambao umeongozwa na Mhe. Zhang Pend, Naibu Meya wa Serikali ya Wananchi ya Jiji la Heze.

Katika mazungumzo yao Bi. Latifa ameeleza jinsi ambavyo TanTrade imekuwa ikishirikiana na China kupitia Kampuni na taasisi mbalimbali ambazo hushiriki katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam (DITF). Mkurugenzi Mkuu ameishukuru Serikali ya China kwa kuweka kipaumbele katika kuhamasisha wafanyabiashara wa China kushiriki katika maonesho ya 48 ambayo yanategemewa kuwa yenye utofauti mkubwa hasa katika eneo la teknolojia ambazo China pia wanategemea kuzileta nchini ambazo zitasaidia kuongeza uzalishaji na thamani ya bidhaa za Tanzania.

Kwa upande mwingine Mhe. Zhang Pend, ameishukuru TanTrade kwa ushirikiano ambao imeendelea kutoa kwa China.
Aidha ujumbe huu pia umeonesha nia ya kufanya biashara na Tanzania hasa katika eneo la bidhaa za Kilimo zikiwemo parachichi, mbolea na nguo,  Magari na vipuri, Vifaa vya ujenzi pamoja na dawa za asili (bio medicine).