Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE YAPONGEZWA KWA UBUNIFU WA PROGRAMU YA URITHI WETU

  • August 30, 2024

22 Agosti,2024.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mwanaisha Khamis Juma  ameipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE)  kwa ubunifu wa programu ya Urithi Wetu , ambayo inalenga kuwasafirisha wanafunzi mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani kutembelea na kujifunza kipindi cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba. Ziara ya kamati hii iliyolenga kutoa uelewa juu ya majukumu mbalimbali ya TanTrade iliyofanyika katika ofisi za mamlaka hiyo zilizopo katika Kiwanja cha J K Nyerere Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Aidha kamati hiyo  imeweza kujifunza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na utafutaji wa masoko na huduma zinazozalishwa Tanzania, kuratibu na kusimamia mifumo ya biashara ili kufanikisha mauzo ya bidhaa na huduma za masoko ya ndani na nje ya nchi, namna ya  kuboresha na kuimarisha taratibu za utoaji huduma, Uwekezaji katika Taasisi, pamoja