Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

TANTRADE KWA KUSHIRIKIANA NA KITUO CHA KIMATAIFA CHA BIASHARA (ITC) YARATIBU MAFUNZO YA MFUMO WA TANZANIA TRADE PORTAL

  • April 25, 2024

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) kwa kushirikiana na Kituo cha Kimataifa cha Biashara (ITC) kupitia mradi wa MARKUP II imeratibu mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa wa TanTrade na Wajumbe wa Kamati ya Uwezeshaji Biashara katika kuingiza, Kuhuisha, na Kurahisisha taarifa za taratibu za kufanya biashara kimataifa katika mfumo wa Uriah’s (Tanzania Trade Portal) mafunzo hayo yametolewa mkoani Morogoro tarehe 22 hadi 25, 2024.

Ambapo Lengo la mafunzo hayo ni kurahisisha taratibu za kibiashara za mazao ya Kahawa, Viungo na Parachichi ili kuona namna ya kurahisisha na kuzipunguzia taratibu za kufanya biashara kimataifa na kuzifanya kuwa na unafuu wa uendeshaji wa biashara, pia kuongeza uwazi na wigo wa  biashara kimataifa